Kuhusu Nichangie

Tanzania ina utamaduni wa kipekee wa kusaidiana — michango ya harusi, misiba, matibabu na ada za shule imekuwa nguzo ya jamii zetu kwa vizazi. Nichangie inachukua utamaduni huo na kuupeleka kidijitali.

Badala ya kuzunguka na daftari la michango au kutegemea makundi ya WhatsApp yasiyo na uwazi, Nichangie inakupa ukurasa mmoja unaoonyesha kila senti iliyokusanywa, nani amechangia na kiasi kilichobaki kufikia lengo.

Michango yote hupitia mifumo salama ya malipo ya mtandao wa simu — M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money na HaloPesa — hivyo mchangiaji hahitaji kadi ya benki wala akaunti mpya.

Uwazi

Kila mchango unaonekana kwenye ukurasa wa mchango kwa muda halisi.

Usalama

Michango hupitia washirika waliosajiliwa wa malipo Tanzania.

Urahisi

Hakuna programu ya kupakua — inatosha link moja tu.

Anzisha mchango wako